Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kusafiri Katika Bahari Kubwa

Kusafiri Katika Bahari Kubwa

Kusafiri Katika Bahari Kubwa

KATIKA Visiwa vya Marshall kuna visiwa vikubwa na vidogo zaidi ya 1,200 hivi, na vingi vimeinuka kidogo tu juu ya usawa wa bahari. Hata mtu anapokuwa baharini mbali kidogo na visiwa hivyo hawezi kuviona. Hata hivyo, mabaharia wa zamani wa Visiwa vya Marshall, waliweza kusafiri kwa mitumbwi kutoka kisiwa kimoja kidogo hadi kingine, katika eneo la Bahari ya Pasifiki lenye ukubwa wa kilometa milioni mbili hivi za mraba. Walifanyaje hivyo? Waliongozwa na “ramani” rahisi, lakini zilizo sahihi, ambazo ziliitwa chati za vijiti.

Kupitia uzoefu, manahodha wa Visiwa vya Marshall walitambua kwamba mahali penye nchi kavu hufanya mawimbi yawe na miundo fulani ambayo huonyesha kuna kisiwa kilometa 30 kutoka kwenye mawimbi hayo. Kulikuwa na miundo mingi ya mawimbi, na chati za vijiti ziliwasaidia manahodha hao kukumbuka miundo hiyo. Chati za vijiti zilikuwaje? Kama unavyoona kwenye picha, vijiti vilivyotengenezwa kutokana na mizizi ya miti fulani au makuti vilifungwa pamoja kufanyiza kiunzi kilichowakilisha miundo ya mawimbi. Makombe madogo yalifungiliwa kwenye kiunzi hicho kuonyesha mahali penye visiwa.

Kwa miaka mingi, ujuzi wa kusafiri kwa mwongozo wa chati za vijiti ulikuwa siri iliyofunuliwa tu kwa watu fulani waliochaguliwa. Nahodha mpya angeweza kujifunzaje kutumia chati ya kijiti? Kwa kuzoezwa na kufanya mazoezi. Nahodha mwenye uzoefu alimfunza nahodha mpya faraghani, labda kwa kusafiri pamoja naye kwenye visiwa vya karibu. Nahodha huyo mpya alipojifunza kutambua miundo ya mawimbi, alipata uhakika wa kutumia chati yake ya kijiti. Baada ya muda, angeweza kusafiri baharini akiwa peke yake.

Vivyo hivyo, Neno la Mungu, Biblia, linaweza kutuongoza maishani. Mwanzoni, huenda mtu fulani akatusaidia kupata ujuzi wa msingi wa Maandiko. Kisha, tunapoendelea kujifunza Neno la Mungu na kutumia kanuni zake, tunaamini yale linalosema. Yoshua, kiongozi wa Waisraeli, aliambiwa aendelee kusoma Neno la Mungu ili ‘apate kuangalia kufanya kulingana na yote ambayo yameandikwa ndani yake.’ Halafu, Mungu akamwambia Yoshua hivi: “Ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha utatenda kwa hekima.” (Yoshua 1:8) Naam, Biblia inaweza kutuonyesha njia bora na yenye mafanikio maishani.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

© Greg Vaughn