NOVEMBA 8, 2019
FILIPINO
Manila, Ufilipino—Kusanyiko la Kimataifa la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
Tarehe:Novemba 1-3, 2019
Mahali: Uwanja wa Mall of Asia Arena and SMX Convention Center huko Manila, Ufilipino
Lugha ya Programu: Kiingereza, Kitagalogi
Idadi ya Wahudhuriaji: 26,245
Idadi ya Waliobatizwa: 145
Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,397
Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Afrika Kusini, Australasia, Indonesia, Italia, Japani, Kazakhstan, Madagaska, Malasia, Marekani, Myanmar, Papua New Guinea, Sri Lanka, Taiwan, Thailand, Ufaransa, Ulaya ya Kati, Visiwa vya Solomon
Mambo Yaliyoonwa:Rogelio Jolongbayan, meneja wa mkoa wa uhusiano na wateja katika uwanja wa Mall of Asia Arena, alisema hivi: “Ninyi ndio kundi lenye utaratibu zaidi kati ya makundi yote ambayo tumewahi kushirikiana nayo. Tumefurahia sana kuwa nanyi katika uwanja wetu.”
Nolasco Bathan, jenerali-brigedia na mkurugenzi wa wilaya wa polisi wa kanda ya kusini alisema hivi: “Wahudhuriaji wote walipanga mstari kwa utaratibu walipokuwa wakiingia uwanjani. Kukiwa na utaratibu mzuri hivi, hatuhitaji kuwa hapa!”
Teofilo Labe Jr., meneja msaidizi wa hoteli ya Manila Hotel alipewa kazi ya kusimamia safari za wajumbe. Baada ya kuwaangalia kwa muda fulani, alisema hivi: “Nikiulizwa na wasimamizi niwape alama kulingana uwezo wenu wa kupanga safari, . . . nitawapa alama ya juu zaidi. Kikundi chenu kina utaratibu mzuri sana.”
Ndugu na dada wenyeji wakiwakaribisha wajumbe kwenye Betheli ya Ufilipino
Ndugu na dada wakigawa mialiko kabla ya kusanyiko
Kabla ya kusanyiko kuanza, wawakilishi wanne wa ofisi ya tawi wakijibu maswali katika mkutano na waandishi wa habari
Wahudhuriaji wa kusanyiko wakiwa nje ya uwanja wa kusanyiko
Wajumbe kutoka mataifa mbalimbali wakipiga picha na ndugu na dada wenyeji
Ndugu na dada wakiimba wimbo wa Ufalme wakati wa kusanyiko
Ndugu wawili wabatizwa siku ya Jumamosi
Ndugu Mark Sanderson, mshiriki wa Baraza Linaloongoza, akitoa hotuba ya mwisho siku ya Jumamosi
Watumishi wa pekee wa wakati wote wakijiunga na Ndugu Sanderson jukwaani na karibu na jukwaa siku ya mwisho ya kusanyiko
Katika tafrija ya jioni, ndugu na dada wakitumbuiza kwa dansi ya asili ya Ufilipino inayoitwa Tinikling