MEI 29, 2019
MAREKANI
Atlanta, Marekani—Kusanyiko la Kimataifa la 2019 la “Upendo Haushindwi Kamwe”!
Tarehe: Mei 17-19, 2019
Mahali: Uwanja wa Mercedes-Benz Atlanta, Georgia, Nchini Marekani
Lugha ya Programu: Kiamhara, Kiingereza, Kirusi
Idadi ya Wahudhuriaji: 46,374
Idadi ya Waliobatizwa: 314
Idadi ya Wajumbe Kutoka Mataifa Mbalimbali: 5,000
Ofisi za Tawi Zilizoalikwa: Australasia, Brazili, Uingereza, Kanada, Chile, Kolombia, Ethiopia, Finland, Ufaransa, Ugiriki, Hong Kong, Israel, Italia, Japani, Kazakhstan, Uholanzi, Ureno, Romania, Skandinavia, Trinidad na Tobago
Haya ni mambo makuu ya kwanza na picha kwenye mfululizo wa makala 24 zitakazochapishwa katika sehemu ya Habari ya jw.org yatakayotolewa kila baada ya kusanyiko la kimataifa mwaka wa 2019.
Kikundi cha Mashahidi wakipiga picha nje ya eneo la kusanyiko
Ndugu Stephen Lett, mshiriki wa Baraza Linaloongoza akitoa hotuba ya mwisho siku ya Jumamosi
Ndugu wakiwabatiza watu katika dimbwi moja kati ya madimbwi mawili yaliyotumiwa kwa ajili ya kusanyiko
Ndugu na dada wakisikiliza programu ya kusanyiko
Baadhi ya watumishi 164 wa pekee wakitembea uwanjani wakati wa sehemu ya mwisho Jumapili
Wajumbe wakiwa kwenye huduma ya shambani pamoja na ndugu na dada wenyeji
Wajumbe wakiwa na nguo za kitamaduni wakipiga picha
Vijana Mashahidi wakiwa wameshika bango linalosema: “Tutakutana Hivi Karibuni Paradiso”
Siku ya mwisho ya kusanyiko, wajumbe wakiwa wamevaa nguo za kitamaduni za Ethiopia
Watumbuizaji wakiwasalimu wahudhuriaji baada ya kuwatumbuiza jioni moja, maneno “Tunawapenda!” yanaonekana upande wa nyuma