Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 8, 2017
MAREKANI

Habari Kuhusu Kimbunga Irma

Habari Kuhusu Kimbunga Irma

Dhoruba iliyofika kwenye nchi kavu Septemba 5, 2017, ni mojawapo ya vimbunga vikubwa zaidi kuwahi kupimwa huko Atlantiki. Imesababisha uharibifu mkubwa kwenye visiwa vingi vya Karibea. Kufikia wakati huu, hakuna ndugu au dada walioripotiwa kufa au kujeruhiwa katika dhoruba hiyo. Jumba moja la Ufalme katika eneo la La Désirade, Guadeloupe; na lingine katika St. Barts; na Jumba la kusanyiko la St. Martin yanahitaji kufanyiwa marekebisho.

Kisiwa cha Barbuda kiliathiriwa sana na dhoruba, asilimia 50 ya wakaaji wamepoteza makao. Watu wote wanaokaa humo kutia ndani ndugu zetu 11 wameagizwa na serikali wahamie Antigua kwa sababu kuna uwezekano wa kimbunga kingine kinachoitwa José, kupiga eneo la Karibea wakati wa mwisho-juma.

Ndugu wamechukua hatua kadhaa za kutoa msaada Kimbunga Irma kinapoelekea upande wa Kaskazini kupitia Bahamas, Kuba, na kusini mashariki ya Marekani. Hilo linatia ndani kutafuta nyumba kwa ajili ya ndugu na dada ambao huenda wakapoteza makao.

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, simu +1-845-524-3000