Hamia kwenye habari

OKTOBA 24, 2016
MAREKANI

Mashahidi Wapanga Kazi Kubwa ya Kutoa Msaada Baada ya Kimbunga Matthew

Mashahidi Wapanga Kazi Kubwa ya Kutoa Msaada Baada ya Kimbunga Matthew

Mashahidi wa Yehova wanajitahidi kuwasaidia waabudu wenzao na waathiriwa wengine wa Kimbunga Matthew, kilichoikumba nchi ya Bahamas, visiwa vya Karibea, na kusini-mashariki mwa Marekani mwanzoni mwa Oktoba 2016.

Karibu nusu ya Mashahidi wa Yehova 1,400 nchini Bahamas waliathiriwa na kimbunga hicho. Chakula, maji, na vifaa vingine walivyohitaji vilipelekwa katika maeneo mawili ili kushughulikia mahitaji yao.

Nchini Kuba, jumla ya nyumba 124 za Mashahidi ziliharibiwa vibaya na 31 zilibomoka kabisa.

Kimbunga hicho kiliwaacha Mashahidi wa Yehova 700 nchini Haiti bila makao. Jumla ya nyumba 73 za Mashahidi na majengo yao manne ya ibada yalibomoka kabisa. Isitoshe, nyumba 274 na majengo 15 ya ibada yaliharibiwa. Chakula na dawa zilisambazwa kwa waathiriwa, na mahema yalinunuliwa ili kuwapa makazi ya muda wale walioachwa bila makao.

Nchini Marekani, kimbunga hicho kiliharibu nyumba 125 za Mashahidi. Ripoti zinaonyesha kwamba kulikuwa na hatari kubwa ya kukumbwa na mafuriko kutokana na mito iliyokuwa imefurika.

Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova linasimamia kazi ya kutoa misaada wakati wa msiba likiwa katika makao makuu yao, kwa kutumia pesa zilizochangwa kwa ajili ya kazi ya Mashahidi ya kuhubiri ya ulimwenguni pote. Msemaji wa Mashahidi wa Yehova, David A. Semonian, anasema: “Ingawa hakuna Shahidi aliyekufa, tunawahurumia wale waliowapoteza wapendwa wao katika msiba huu.”

Wanahabari Wanaweza Kuwasiliana na:

David A. Semonian, Ofisi ya Habari za Umma, 1-718-560-5000

Bahamas: Maxwell Dean, 1-242-422-6472

Haiti: Daniel Lainé, 509-2813-1560