Hamia kwenye habari

AGOSTI 11, 2017
TAIWAN

Programu Yenye Mafanikio ya Utumishi wa Badala wa Kiraia Nchini Taiwan

Programu Yenye Mafanikio ya Utumishi wa Badala wa Kiraia Nchini Taiwan

Mwaka 2000, Taiwan ilitekeleza programu ya utumishi wa badala wa kiraia ambao uliwaruhusu wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri kutimiza wajibu wao wa kufanya utumishi wa taifa bila kukiuka dhamiri zao. Chini ya mpango huu, wale wanaokataa kujiunga na utumishi wa kijeshi kwa sababu ya dhamiri wamekuwa wakipewa nafasi ya kutumikia ama katika hospitali, kufanya kazi kwenye nyumba za kuwatunzia wazee, au maeneo mengine ya umma. Programu hii imepata mafanikio mengi sana, imewanufaisha watu wa Taiwan na wale wanaokataa kujiunga na jeshi kwa sababu ya dhamiri ambao sasa hawakabili kifungo kwa sababu ya msimamo wao wa kutounga mkono upande wowote.

Video hii inaeleza jinsi programu ya utumishi wa badala wa kiraia ulivyotekelezwa nchini Taiwan, inajibu maswali ambayo mara nyingi yanajitokeza kwa wale wanaopinga mpango huu, na ina maelezo ya wale waliohusika kwenye mpango huu. Bw. Kuo-Enn Lin, msimamizi mkuu wa National Conscription Agency, alisema hivi: “Ninatumaini kwamba nchi nyingine zitatutembelea na kujifunza kutokana na mfano wetu.”