OKTOBA 21, 2021 | TAREHE YA KARIBUNI: DESEMBA 26, 2022
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—ADHABU YAONGEZWA | Wana Shangwe Licha ya Kuwekwa Mahabusu na Kuwa Katika Kifungo cha Nyumbani kwa Muda Mrefu
Desemba 22, 2022, Mahakama ya Nne ya Kuchunguza Maamuzi ya Mahakama za Chini iliongeza adhabu waliyopewa Ndugu Rustam Diarov na Ndugu Sergey Klikunov, pamoja na Ndugu Yevgeniy Ivanov na mke wake, Olga. Hakimu alitangaza kwamba baada ya kumaliza kutumikia vifungo vyao, hawataruhusiwa kuondoka katika eneo la Astrakhan kwa sababu yoyote ile. Ndugu hao watatu pamoja na dada yetu walishiriki katika kesi yao kupitia video iliyounganishwa kupitia mtandao huku wakiwa mahabusu.
Machi 3, 2022, Mahakama ya Eneo la Astrakhan ilitupilia mbali ombi la rufaa la Ndugu Rustam Diarov na Sergey Klikunov, na Ndugu Yevgeniy Ivanov na mke wake, Olga. Wote wanne wataendelea kukaa gerezani.
Mfuatano wa Matukio
Oktoba 25, 2021
Mahakama ya Wilaya ya Trusovskiy iliyo Astrakhan iliwahukumu Rustam, Yevgeniy, na Sergey miaka minane gerezani. Olga, mke wa Yevgeniy, alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu na miezi sita gerezani. Ndugu hao watatu tayari walikuwa mahabusu. Dada Olga alipelekwa kizuizini mara moja
Juni 11, 2020
Rustam, Yevgeniy, na Sergey waliwekwa mahabusu katika sehemu nyingine. Olga alifungwa kifungo cha nyumbani
Juni 9, 2020
Zaidi ya maofisa 100 wa usalama walivamia nyumba za familia 27 za Mashahidi wa Yehova katika jiji la Astrakhan. Rustam, Yevgeniy, Olga, na Sergey waliwekwa mahabusu
Juni 8, 2020
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Rustam, Yevgeniy, Olga, na Sergey. Akina ndugu wote walishtakiwa kwamba wanapanga na kutegemeza kifedha utendaji wenye msimamo mkali. Olga alishtakiwa kwa kushiriki katika utendaji wenye msimamo mkali
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Inafariji sana kujua kwamba sikuzote Yehova yuko karibu na watumishi wake washikamanifu wanapopatwa na majaribu.—Zaburi 139:5, 10.