MEI 6, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: FEBRUARI 21, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—DADA AHUKUMIWA | Tatyana Obizhestvit Anamtumaini Yehova
Februari 20, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Vakhitovskiy iliyo Kazan katika Jamhuri ya Tatarstan ilimhukumu Dada Tatyana Obizhestvit kifungo cha nje cha miaka miwili. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Mfuatano wa Matukio
Januari 19, 2020
Wenye mamlaka walipekua nyumba ya Tatyana na nyumba nyingine kadhaa za Mashahidi wa Yehova huko Kazan. Tatyana alihojiwa kisha akapelekwa mahabusu
Januari 21, 2020
Aliachiliwa na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani
Mei 25, 2021
Kesi ya uhalifu ilianza
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunathamini sana mfano wa Tatyana wa kumtumaini Yehova na kuepuka kutegemea uelewaji wake mwenyewe huku akiendelea kuvumilia kwa uaminifu.—Methali 3:5.