AGOSTI 26, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: MACHI 8, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU YABADILISHWA | Wavumilia Mateso kwa Utulivu na Uhakika
Machi 1, 2023, Mahakama ya Eneo la Stavropol ilitangaza uamuzi wake katika kesi inayowahusu Ndugu Anatoliy na mke wake, Irina, na pia Ndugu Viktor Zimovskiy. Vifungo ambavyo Anatoliy na Viktor walikuwa wamepewa hapo awali vimebadilishwa vikawa vifungo vya nje. Anatoliy hahitaji kwenda kwenye kambi ya kurekebisha tabia. Viktor aliachiliwa mara moja. Kifungo cha nje cha Irina hakijabadilishwa. Irina hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Novemba 14, 2022, Mahakama ya Jiji la Georgievskiy iliyo katika Eneo la Stavropol iliwahukumu Anatoliy na mke wake, Irina, pamoja na Viktor. Anatoliy alihukumiwa kifungo cha miaka minne na miezi miwili katika kambi ya kurekebisha tabia. Irina alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka minne na miezi miwili. Viktor alihukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi miwili gerezani na alipelekwa gerezani moja kwa moja.
Mfuatano wa Matukio
Oktoba 23, 2019
Maofisa wa polisi walifanya msako kwenye nyumba za familia tatu za Mashahidi wa Yehova katika mji wa Georgievsk. Walipokuwa wakifanya msako kwenye nyumba hizo, kwa ulaghai maofisa hao waliweka humo vitu mbalimbali ambavyo walikusudia kutumia kama ushahidi wa uwongo. Anatoliy, Irina, Viktor, na Mashahidi wengine nane walizuiliwa na kuhojiwa usiku mzima
Desemba 30, 2019
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Anatoliy, Irina, na Viktor
Januari 23, 2020
Viktor aliitwa tena ili akahojiwe, kisha akazuiliwa. Siku iliyofuata, alihamishwa kutoka kwenye sehemu aliyokuwa amezuiliwa na akapelekwa mahabusu
Machi 23, 2020
Viktor aliachiliwa kutoka mahabusu na akawekwa kwenye kifungo cha nyumbani
Mei 6, 2020
Viktor aliachiliwa kutoka kwenye kifungo cha nyumbani na akawekewa vizuizi vya kusafiri
Oktoba 6, 2021
Viktor aliondelewa vizuizi vya kusafiri
Machi 10, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Tunaamini kwamba Yehova ataendelea kuwa “karibu na wote wanaomwitia” wanapovumilia wakiwa na shangwe na tumaini.—Zaburi 145:18.