APRILI 8, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: JULAI 1, 2024
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—HUKUMU ZA GEREZANI | Wanauona Mkono wa Yehova Wakiwa Mahabusu
Juni 26, 2024, Mahakama ya Jiji la Novocherkassk iliyo katika Eneo la Rostov iliwahukumu Dada Lyubov Galitsyna, Ndugu Garegin Khachaturyan, na Ndugu Gevorg Yeritsyan. Dada Lyubov alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na miezi mitatu gerezani, lakini kwa kuwa amekuwa katika kifungo cha nje, kifungo chake kimekamilika. Ndugu Garegin alihukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi sita na Ndugu Gevorg akahukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi miwili gerezani. Ndugu wote wawili wataendelea kukaa kifungoni.
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Tuna uhakika kwamba ingawa wapinzani wetu wameazimia kutudhuru, Yehova ataendelea kuwabariki watumishi wake washikamanifu na kufanya “hali hiyo ibadilike na kuwa njema.”—Mwanzo 50:20
Mfuatano wa Matukio
Agosti 11, 2022
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Lyubov, Garegin, na Gevorg. Nyumba zao zilifanyiwa msako. Garegin na Gevorg waliwekwa kizuizini
Agosti 12, 2022
Garegin na Gevorg walihamishiwa mahabusu
Agosti 16, 2022
Lyubov aliwekwa kizuizini
Agosti 17, 2022
Lyubov alihamishiwa mahabusu
Septemba 20, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza
Desemba 25, 2023
Lyubov alitolewa mahabusu na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani