Hamia kwenye habari

Kutoka kushoto hadi kulia: Ndugu Denis Filatov, Ndugu Stanislav Klyuchnikov, na Ndugu Dmitriy Yarchak

JUNI 1, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: SEPTEMBA 6, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAHUKUMIWA | Wanaendelea Kuwa Imara kwa Sababu Yehova Yuko Upande Wao

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAHUKUMIWA | Wanaendelea Kuwa Imara kwa Sababu Yehova Yuko Upande Wao

Septemba 5, 2023, Mahakama ya Jiji la Nizhnekamsk iliyo katika Jamhuri ya Tatarstan iliwahukumu Ndugu Denis Filatov, Ndugu Stanislav Klyuchnikov, na Ndugu Dmitriy Yarchak kifungo cha nje cha miaka sita kila mmoja. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Novemba 18, 2020

    Maofisa wa FSB pamoja na maofisa wengine wa polisi waliobeba silaha walivamia nyumba 12 za Mashahidi wa Yehova katika jiji la Nizhnekamsk. Ndugu tisa na dada watatu walipelekwa kituoni ili wakahojiwe

  2. Agosti 24, 2021

    Baada ya kuhojiwa, Denis, Stanislav, na Dmitriy waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  3. Oktoba 7, 2021

    Denis, Stanislav, na Dmitriy walishtakiwa kwa madai kwamba ‘waliimba nyimbo za kipekee za kidini na kusali’

  4. Januari 27, 2022

    Kesi hiyo ya uhalifu ilianza kusikilizwa upya kwenye Mahakama ya Jiji la Nizhnekamsk iliyo katika Jamhuri ya Tatarstan

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Ndugu zetu wanaendelea kumtegemea Yehova awape nguvu na hatuna shaka kwamba wanahisi kama alivyohisi mtunga zaburi Daudi aliyesema: “Nina hakika kuhusu jambo hili: Mungu yuko upande wangu.”​—Zaburi 56:9.