JANUARI 13, 2022
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI | Uhakika Katika Yehova Unamsaidia Ndugu Yevstigneev Kudumisha Uaminifu
Agosti 1, 2022, Mahakama ya Eneo la Nizhny Novgorod ilikataa ombi la rufaa la Ndugu Kirill Yevstigneev. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Mei 12, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy iliyo katika Jiji la Nizhny Novgorod ilimhukumu Kirill kifungo cha nje cha miaka mitatu.
Mfuatano wa Matukio
Oktoba 8, 2021
Kesi ya uhalifu ilianza. Katika maelezo yake kwa hakimu, Kirill alieleza kwamba kikusanyiko hicho hakikuwa cha kidini bali kikusanyiko cha kirafiki
Agosti 24, 2021
Kirill aliwekewa vizuizi vya kusafiri
Septemba 2, 2020
Kesi ya uhalifu ilianzishwa dhidi ya Kirill na akashtakiwa “kuunga mkono kifedha utendaji wenye msimamo mkali” kwa sababu alikodisha chumba cha mkutano
Julai 11, 2019
Wenye mamlaka walimkazia fikira Kirill kwa sababu yeye ndiye aliyetia sahihi mkataba kwa ajili ya chumba cha mkutano; nyumba yake ilifanyiwa upekuzi
Juni 4, 2019
Uchunguzi ulianzishwa dhidi ya “watu wasiotambulishwa” kwa sababu ya kikusanyiko hicho
Aprili 2019
Kirill na baadhi ya Mashahidi wa Yehova katika Nizhny Novgorod walikodi chumba cha mkutano kwa ajili ya kikusanyiko cha kirafiki
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunaendelea kuwa na uhakika tunaposikia kuhusu ujasiri ambao Kirill, mke wake, na ndugu na dada wote waaminifu nchini Urusi na Crimea wanaonyesha licha ya mateso wanayokabili.—Wafilipi 1:13, 14.