APRILI 1, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: JULAI 30, 2024
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—WATATU WAMEHUKUMIWA | “Sitavunja Utimilifu Wangu”
Julai 30, 2024, Mahakama ya Jiji la Nikolaevsk-on-Amur iliyo katika Eneo la Khabarovsk ilimhukumu Ndugu Igor Kletkin na Ndugu Nikolay Kononenko kifungo cha nje cha miaka sita. Dada Nadezhda Korobochko alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitano. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Tunamshukuru Yehova kwa kuwatunza kwa upendo na na kuwategemeza wote wanaomtumaini na kutangaza: “Wewe ni Mungu wangu.”—Zaburi 31:14.
Mfuatano wa Matukio
Oktoba 11, 2021
Nyumba ya Igor na ya Nadezhda zilifanyiwa msako. Igor aliwekwa kizuizini
Oktoba 12, 2021
Nadezhda alihojiwa
Oktoba 13, 2021
Igor aliachiliwa kutoka kizuizini
Oktoba 14, 2021
Igor na Nadezhda waliwekewa vizuizi vya kusafiri
Septemba 27, 2022
Nikolay aliwekewa vizuizi vya kusafiri
Januari 16, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza