MACHI 24, 2022
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI | Yehova Anaendelea Kutegemeza Familia za Ndugu Sita Walio Mahabusu
Septemba 19, 2022, Mahakama ya Jiji la Gukovo iliyo katika Eneo la Rostov iliwahukumu Ndugu Aleksey Dyadkin, Ndugu Aleksey Goreliy, Ndugu Nikita Moiseyev, Ndugu Vladimir Popov, Ndugu Yevgeniy Razumov, na Ndugu Oleg Shidlovskiy. Ndugu Goreliy na Ndugu Shidlovskiy walihukumiwa kifungo cha miaka sita na nusu gerezani. Ndugu Dyadkin, Ndugu Moiseyev, Ndugu Popov, na Ndugu Razumov walihukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani. Hukumu hizo zitatekelezwa mara moja.
Mfuatano wa Matukio
Agosti 8, 2020
Maofisa wa FSB walifanya msako katika nyumba 17 za Mashahidi wa Yehova katika majiji matatu katika Eneo la Rostov na katika jiji la Kursk. Ndugu Goreliy, Ndugu Moiseyev, Ndugu Razumov, na Ndugu Shidlovskiy walikamatwa na kisha siku iliyofuata walipelekwa mahabusu. Ndugu Popov aliwekwa kwenye orodha ya wahalifu nchini
Agosti 12, 2020
Maofisa wa FSB walimweka Ndugu Popov kizuizini. Kisha baada ya siku mbili alipelekwa mahabusu
Agosti 21, 2020
Baada ya Ndugu Dyadkin kuhojiwa na wenye mamlaka alipelekwa mahabusu
Juni 28, 2021
Wakili aliwatembelea ndugu hao sita wakiwa mahabusu. Walimweleza kuhusu hali ngumu wanazopitia, kama vile joto kali lililozidi nyuzi 40 Selsiasi, kuvu kwenye kuta, na kuwekwa pamoja na wafungwa walio na COVID-19
Julai 21, 2021
Ndugu Popov alikuwa na matatizo ya kupumua, basi alihamishwa na kupelekwa kwenye mahabusu nyingine yenye kituo cha matibabu. Baada ya muda alipelekwa hospitali
Septemba 30, 2021
Ndugu Popov alirudishwa mahabusu baada ya kuwa hospitali kwa zaidi ya miezi miwili
Novemba 17, 2021
Kesi ya uhalifu ilianza, na ndugu hao sita wakaongezewa muda wa kukaa mahabusu
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Tunaendelea kumwomba Yehova kwa bidii awasaidie ndugu hao na familia zao. Tuna uhakika kwamba Yehova atawapa imani na nguvu wanazohitaji.—Waroma 15:30.