JULAI 8, 2022
URUSI
Kupata Nguvu Kupitia Sala
Mahakama ya Wilaya ya Pervomayskiy iliyo Izhevsk itatangaza uamuzi wake hivi karibuni katika kesi inayomhusu Ndugu Sergey Ashikhmin, Ndugu Maksim Derendyaev, na Ndugu Aleksandr Kutin. Mwendesha mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.
Mfuatano wa Matukio
Aprili 14, 2021
Maofisa wa FSB walifanya msako kwenye nyumba 12 hivi za Mashahidi wa Yehova. Sergey alihojiwa kwa saa saba. Maksim na Aleksandr walikamatwa na kupelekwa gerezani
Aprili 15, 2021
Maksim na Aleksandr walipelekwa mahabusu
Aprili 29, 2021
Aleksandr aliachiliwa kutoka mahabusu
Mei 14, 2021
Aleksandr aliwekwa katika kifungo cha nyumbani
Julai 9, 2021
Maksim aliachiliwa kutoka mahabusu na kuwekwa kwenye kifungo cha nyumbani
Machi 14, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Ndugu zetu wanaendelea kukabiliana na ukosefu wa haki wakiwa na uhakika katika Yehova ambaye anatuahidi: “Usiogope, kwa maana nipo pamoja nawe.”—Isaya 43:5.