Hamia kwenye habari

Ndugu Konstantin Bazhenov

OKTOBA 28, 2020
URUSI

Mahakama ya Urusi Yakataa Kumwachilia Mapema Ndugu Bazhenov

Mahakama ya Urusi Yakataa Kumwachilia Mapema Ndugu Bazhenov

Oktoba 28, 2020, Mahakama ya Jiji la Dimitrovgrad ya Eneo la Ulyanovsk ilikataa kumwachilia mapema Ndugu Konstantin Bazhenov na kubadilisha muda uliosalia wa kifungo chake kuwa faini. Ana siku kumi za kukata rufaa.

Mwanzoni, Ndugu Bazhenov aliogopa alipopelekwa mahabusu mnamo Juni 2018. Hata hivyo, alianza kuandika mistari ya Biblia katika kitabu. Alifaulu kuandika mistari 500 hivi aliyokumbuka. Hatimaye, alipata Biblia na akaisoma ndani ya miezi minne. Ndugu Bazhenov aliandika barua zilizokuwa na mawazo ya Kimaandiko ili kuwatia moyo wengine. Pia, aliimba nyimbo za Ufalme na alimtolea Yehova dua mara nyingi akimwomba msaada.

Ndugu Bazhenov alikaa mahabusu kwa zaidi ya siku 340. Baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu na nusu gerezani mnamo Septemba 2019, aliendelea na ratiba yake ya kiroho. Yehova alimwezesha Ndugu Bazhenov kuadhimisha Ukumbusho akiwa gerezani. Kwa kuendelea kukaa karibu na Yehova, Ndugu Bazhenov amefaulu kuvumilia mateso kwa shangwe. Sisi sote na tuendelee kumkumbuka Ndugu Bazhenov katika sala zetu.