OKTOBA 1, 2021
URUSI
Ndugu Watano Wameazimia Kuvumilia Licha ya Mateso
Mfuatano wa Matukio
Mahakama ya Wilaya ya Industrialniy iliyoko Orenburg itatangaza hivi karibuni uamuzi katika kesi inayohusu Ndugu Vladimir Kochnev, Ndugu Vladislav Kolbanov, Ndugu Pavel Lekontsev, Ndugu Sergey Logunov, na Ndugu Nikolay Zhugin. a Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza
Machi 1, 2021
Zaidi ya mwaka mmoja baada ya kesi hiyo kurudishwa kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka, kesi ilianza kusikilizwa katika Mahakama ya Wilaya ya Industrialniy iliyoko Orenburg
Januari 14, 2020
Kesi ya uhalifu ilirudishwa kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka kwa sababu mashtaka hayakuwa wazi
Agosti 3, 2018
Vladimir aliachiliwa kutoka mahabusu baada ya siku 79 na akawekwa chini ya kifungo cha nyumbani
Mei 16, 2018
Wenye mamlaka walifanya upekuzi katika nyumba za familia 19 katika Eneo la Orenburg. Vladimir na Vladislav walipelekwa mahabusu. Vladislav aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani siku tatu baadaye
Mei 14, 2018
Msimamizi wa Kamati ya Uchunguzi ya Shirikisho la Urusi katika Eneo la Orenburg alifungua kesi ya uhalifu dhidi ya ndugu wote watano
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Hata ingawa kesi dhidi ya imani yao imeendelea kwa zaidi ya miaka mitatu, ni wazi kwamba ndugu zetu wapendwa wameazimia kudumisha ushikamanifu wao kwa Yehova. Ni wazi pia kwamba Yehova anatenda kwa ushikamanifu kuwaelekea.—2 Samweli 22:26.
a Tarehe ya hukumu haitolewi mapema pindi zote