APRILI 6, 2017
URUSI
Mahakama Kuu ya Urusi Itaendelea Kusikiliza Kesi ya Kuwapiga Marufuku Mashahidi wa Yehova Aprili 7
Leo katika Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi kesi ilianza kwa Wizara ya Haki kujadili wazo la kwamba ni lazima mashirika ya kisheria ya Mashahidi wa Yehova yapigwe marufuku kwa sababu mahakama za chini zilifikia uamuzi kwamba baadhi ya mashirika hayo yameshiriki katika utendaji wenye msimamo mkali. Hakimu akamwuliza mwakilishi wa Wizara ya Haki ni jinsi gani matendo ya mashirika 8 tu yaliyoshtakiwa yanavyoweza kutumiwa kuwa msingi wa kufikia uamuzi kama huo dhidi ya Kituo cha Usimamizi na dhidi ya mashirika yote 395 nchini Urusi. Hakimu huyo aliuliza pia kufungwa kwa mashirika yote kutaathirije ibada ya Mashahidi wa Yehova, na akauliza mara nyingi ni jinsi gani Mashahidi ni tisho kwa usalama na kwa jamii. Pia mawakili wa Mashahidi waliuliza maswali yaliyoonyesha wazi kwamba nia ya Wizara ya Haki si kufunga mashirika yao ya kisheria peke yake, bali ni kupiga marufuku dini ya Mashahidi wa Yehova.
Kesi itaendelea Aprili 7, 2017, saa 4:00 asubuhi.