Hamia kwenye habari

APRILI 3, 2017
URUSI

Video: Wataalamu Wazungumzia Tisho la Kuwapiga Marufuku Mashahidi wa Yehova Nchini Urusi

Video: Wataalamu Wazungumzia Tisho la Kuwapiga Marufuku Mashahidi wa Yehova Nchini Urusi

Aprili 5, 2017, Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi inatazamiwa kutoa uamuzi kuhusu kufunga na kupiga marufuku utendaji wa mashirika ya kisheria yanayotumiwa na Mashahidi wa Yehova kotekote nchini Urusi. Uamuzi ukifanywa dhidi ya Mashahidi utamaanisha kwamba ni tendo la uhalifu kwao kuendeleza ibada yao. Wataalamu kadhaa wa haki za kibinadamu nchini Urusi na kutoka nchi nyingine wanazungumzia matendo yasiyo ya haki yanayofanywa na wenye mamlaka nchini Urusi na jinsi ambavyo kupigwa marufuku kwa Mashahidi wa Yehova kutaathiri si Mashahidi tu bali pia sifa ya kimataifa ya Urusi na uhuru wa kidini wa raia wake wote.

  • Heiner Bielefeldt: “Ikiwa Mashahidi wa Yehova wana msimamo mkali, sisi sote pia tuna msimamo mkali”

    Aliyekuwa Msemaji wa Pekee wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Masuala ya Uhuru wa Ibada na Imani

  • Richard Clayton, QC: “Ni mfano wa kushtua wa sheria mbaya inayotumiwa kwa makusudi yasiyofaa.”

    Mwanasheria wa Kimataifa wa Haki za Binadamu na Mwakilishi wa Uingereza Katika Tume ya Venice

  • Dakt. Massimo Introvigne: “Uhusiano pekee uliopo kati ya Mashahidi wa Yehova na jeuri ni kwamba wao ni waathiriwa wa jeuri.”

    Mwanasosholojia na Mwakilishi Mstaafu wa OSCE Katika Kukabiliana na Ubaguzi wa Rangi, wa Kijamii, na Upendeleo

  • Annika Hvithamar: ‘Ikiwa Mashahidi wa Yehova wana msimamo mkali, basi aina nyingi za Ukristo zinapaswa kushtakiwa kuhusu jambo hilo pia.’

    Profesa Msaidizi/Msimamizi wa Mafunzo, Idara ya Mafunzo Kuhusu Tamaduni na Maeneo Mbalimbali, Chuo Kikuu cha Copenhagen

  • Lyudmila Alekseyeva: “Hilo si kosa—Nafikiri ni uhalifu”

    Mwenyekiti wa Kikundi cha Moscow Helsinki, Mshiriki wa Kamati ya Rais wa Urusi Kuhusu Masuala ya Raia na Haki za Kibinadamu

  • Anatoly Vasilyevich Pchelintsev: “Acheni tuwatetee Mashahidi wa Yehova!”

    Mhariri Mkuu wa Jarida Dini na Sheria (Religion and Law)

  • Vladimir Vasilyevich Ryakhovskiy: “Sikuzote shida zimeanza kwa Mashahidi wa Yehova halafu zinaenea kwa kila mtu”

    Mshiriki wa Kamati ya Rais Kuhusu Masuala ya Raia na Haki za Kibinadamu

  • Maksim Shevchenko: “Dai hili linakiuka kanuni za msingi za uhuru wa dhamiri”

    Msimamizi wa Kituo cha Uchunguzi wa Kidini na Watu Mashuhuri wa Kisiasa

  • Dakt. Hubert Seiwert: ‘Mashtaka yote yanayotolewa dhidi ya Mashahidi wa Yehova ambayo husikilizwa mahakamani hayana uthibitisho.’

    Profesa wa Taasisi ya Masomo ya Kidini Katika Chuo Kikuu cha Leipzig

  • Mercedes Murillo Muñoz: “Nchi ina uhakika mkubwa na dhehebu hili.”

    Profesa wa Sheria za Kanisa Katika Chuo Kikuu cha King Juan Carlos (Hispania)

  • Consuelo Madrigal: “Siwaoni [Mashahidi wa Yehova] kuwa watu hatari hata kidogo.”

    Mwanasheria na Wakili Mkuu wa Zamani wa Hispania