Matukio Muhimu Kihistoria Nchini Uzibekistani
FEBRUARI 19, 2009—Serikali yakataa ombi la 16 la kusajili Mashahidi wa Yehova jijini Tashkent. Maombi ya mapema yalikuwa yamekataliwa pia, yalikuwa ya mwaka wa 1997, 1998, 2000, 2001, 2003, 2004, 2005, na wa 2006
AGOSTI 24, 2006—Serikali yafuta usajili wa shirika la LRO jijini Fergana
AGOSTI 1999—Serikali yasajili upya shirika la LRO jijini Chirchik na shirika la LRO jijini Fergana
MEI 1, 1998—Serikali yatoa sheria ya kudhibiti mashirika ya kidini na inayotaka mashirika hayo yajiandikishe upya
DESEMBA 1996—Serikali yakataa ombi la kwanza la kusajiliwa la Mashahidi wa Yehova jijini Tashkent
DESEMBA 17, 1994—Serikali yasajili mashirika ya kidini ya Mashahidi wa Yehova (LRO) katika jiji la Chirchik na Fergana
DESEMBA 8, 1992—Serikali mpya ilitayarisha katiba mpya inayowahakikishia raia haki za msingi za kibinadamu
SEPTEMBA 1, 1991—Uzbekistan yapata uhuru
Miaka ya 1960—Utendaji wa kwanza wa Mashahidi wa Yehova ulioripotiwa Angren na Chirchik