Esta Alimtanguliza Yehova na Watu Wake
Esta alikuwa jasiri na aliwatanguliza wengine alipomtetea Yehova na watu wake
-
Esta na Mordekai walikuwa salama. Lakini agizo la Hamani la kuwaua Wayahudi lilikuwa likisambazwa kotekote katika milki ya Ahasuero
-
Esta alihatarisha uhai wake tena kwa kwenda mbele ya mfalme bila kuitwa. Alilia kwa ajili ya watu wake na kumwomba mfalme afutilie mbali agizo alilokuwa ametoa
-
Sheria zilizopitishwa katika jina la mfalme hazingebadilishwa. Hivyo, mfalme alimpa Esta na Mordekai mamlaka ya kuandika sheria mpya
Yehova aliwapa watu wake ushindi mkubwa
-
Tangazo la pili lilitolewa la kuwapa Wayahudi haki ya kujilinda
-
Wapanda-farasi wakaenda upesi kila sehemu ya milki hiyo na Wayahudi wakajitayarisha kupigana
-
Watu wengi waligeuzwa imani na kuwa wafuasi wa dini ya Wayahudi kwa sababu waliona uthibitisho kwamba Wayahudi wana kibali cha Mungu