“Endeleeni Kukesha”
Ingawa Yesu alielekeza mfano wa mabikira kumi kwa wafuasi wake watiwa-mafuta, ujumbe wake muhimu unawahusu Wakristo wote. (w15 3/15 12-16) “Kwa hiyo, endeleeni kukesha kwa sababu hamjui ile siku wala saa.” (Mt 25:13) Je, unaweza kueleza mfano wa Yesu?
-
Bwana harusi (mst. 1)—Yesu
-
Mabikira wenye busara waliojitayarisha (mst. 2)—Wakristo watiwa-mafuta ambao wamejitayarisha kutimiza mgawo wao kwa uaminifu na ambao wanaangaza daima kama mianga hadi mwisho (Flp 2:15)
-
Mwito: “Huyu hapa Bwana harusi!” (mst. 6)—Uthibitisho wa kuwapo kwa Yesu
-
Mabikira wapumbavu (mst. 8)—Wakristo watiwa-mafuta ambao wanaenda kumpokea Bwana harusi lakini hawaendelei kukesha na hawadumishi utimilifu wao
-
Mabikira wenye busara wanakataa kuwapa wenzao mafuta (mst. 9)—Baada ya muhuri wa mwisho, itakuwa kuchelewa sana kwa watiwa-mafuta waaminifu kuwasaidia wale walioacha kuwa waaminifu
-
“Bwana harusi akaja” (mst. 10)—Yesu anakuja karibu na mwisho wa dhiki kuu ili kuhukumu
-
Mabikira wenye busara wanaingia kwenye karamu ya ndoa pamoja na Bwana harusi, na mlango unafungwa (mst. 10)—Yesu anawakusanya watiwa-mafuta waaminifu kwenda mbinguni, lakini wasio waaminifu wanapoteza thawabu yao ya kwenda mbinguni