Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Ni upi uliokuwa mpaka wa kaskazini wa Bara Lililoahidiwa na mlima mrefu zaidi karibu na Palestina? (Yoshua 12:1)
2. Ni sifa gani aliyo nayo Yehova inayofanya wanadamu watamanike, na ambayo si ishara ya udhaifu? (Zaburi 18:35)
3. Malaika wa Yehova aliwapiga wanajeshi wangapi Waashuri katika usiku mmoja? (2 Wafalme 19:35)
4. Ni nani aliyepaka miguu ya Yesu mafuta ghali sana yenye marashi na kuifuta kwa nywele zake? (Yohana 12:3)
5. Wazalisha Waebrania waliopuuza amri ya Farao ya kuua watoto wanaume na Yehova akawabariki kwa kuwapa familia waliitwaje? (Kutoka 1:15-21)
6. Ni mfalme yupi wa Yuda ambaye licha ya kukosea nyakati nyingine wakati wa utawala wake wa miaka 41, alionwa kuwa mmojawapo wa wafalme waaminifu? (1 Wafalme 15:14, 18)
7. Katika unabii wa kurudishwa, ni mnyama yupi anayesemwa kuwa ‘anakula majani kama ng’ombe’? (Isaya 65:25)
8. Wenyeji wote wa Sodoma, vijana kwa wazee, waliizunguka nyumba ya Loti kwa sababu gani? (Mwanzo 19:4, 5)
9. Katika kujibu sala ya Samweli, Yehova alitumia nini ili kuwafadhaisha Wafilisti hata wakashindwa? (1 Samweli 7:9, 10)
10. Musa alitoa sababu gani alipomwomba Farao awaruhusu Waisraeli waende? (Kutoka 5:1)
11. Ni tawi la mti gani unaozaa matunda linalotumiwa mara nyingi kuashiria amani? (Ona Isaya 17:6.)
12. Kati ya vitabu vitano vya Biblia vilivyoandikwa na Yohana, ni kipi kilichoandikwa kwanza?
13. Mithali husema ni nani aliye “taji kwa mumewe”? (Mithali 12:4)
14. Ajapostahili, ni nani aliyekataa kutuzwa na Mfalme Daudi kwa sababu ya kuwa na umri wa miaka 80? (2 Samweli 19:31-36)
15. Yasemekana Shetani alikuwa ameongoza vibaya idadi gani ya ufananisho ya malaika? (Ufunuo 12:4)
Majibu ya Maswali
1. Mlima Hermoni
2. Unyenyekevu
3. 185,000
4. Maria, dadake Martha na Lazaro
5. Shifra na Pua
6. Asa
7. Simba
8. Walitaka kuwabaka malaika waliomtembelea
9. Ngurumo
10. Ili wakamfanyie Yehova sikukuu jangwani
11. Mzeituni
12. Ufunuo
13. “Mke mwema”
14. Barzilai, Mgileadi kutoka Rogelimu
15. Theluthi