Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Avutiwa na Busara ya Amkeni!

Avutiwa na Busara ya Amkeni!

Avutiwa na Busara ya Amkeni!

PROFESA MMOJA WA CHUO KIKUU nchini Hispania aliandikia Watch Tower Society katika nchi yake ili kuwashukuru kwa ajili ya uchapishaji wa Amkeni! Alieleza hivi:

“Hivi karibuni nilipata nakala mbili za jarida lenu Amkeni! Zilikuwa na makala zenye kupendeza kuhusu habari mbalimbali. Mimi si mfuasi wa dini yoyote, lakini niliweza kuona kwamba gazeti hilo halipendelei upande wowote. Pia lina muundo mzuri sana, na latoa habari kwa njia isiyopendelea na kwa njia ya kisayansi. Nawapongeza kwa jitihada zenu.”

Katika makala nyingi, Amkeni! laonyesha uthibitisho wa kisayansi, ambao huwasaidia wasomaji wake kufanya maamuzi yanayofaa kuhusiana na habari mbalimbali. Broshua Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai? Wewe Waweza Kulipataje? imeandikwa kwa njia hiyohiyo. Kwa mfano, chini ya vichwa vidogo vya “Je, Uhai Ulijitokeza kwa Nasibu?” na “Ubuni Hutaka Mbuni.” Majibu ya masuala hayo yametolewa kulingana na wataalamu wa astronomia, mikrobiolojia, na fizikia.

Waweza kuomba broshua, Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai? Wewe Waweza Kulipataje?, kwa kujaza na kutuma kuponi iliyopo hapa kwa anwani iliyoonyeshwa au kwa anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa gazeti hili.

□ Nitumieni nakala ya broshua Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai? Wewe Waweza Kulipataje? Onyesha lugha unayotaka

□ Tafadhali wasilianeni nami kuhusu funzo la Biblia la nyumbani bila malipo.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Galaxy: Courtesy of Anglo-Australian Observatory, picture by David Malin