Je Wajua?
Je Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Kwa nini ni kosa kujilipizia kisasi au kuwalipizia wengine? (Waroma 12:19)
2. Kwa nini Yehova anakataza ibada ya sanamu au ya mifano? (Isaya 42:8)
3. Yesu aliuonaje mgawo wake wa kidunia aliopewa na Mungu? (Yohana 4:34)
4. Daudi alitiwa mafuta wapi ili awe mfalme, mahali ambapo alikuwa na makao yake makuu kabla ya kuhamia Yerusalemu? (2 Samweli 2:1-4)
5. Kulingana na Yohana, upinde-mvua unaozunguka kiti cha enzi cha Yehova unafanana na jiwe gani la thamani? (Ufunuo 4:3)
6. Paulo huenda alisimama mahali gani alipokuwa akipelekwa Roma akiwa mfungwa? (Matendo 28:13)
7. Ni usemi gani wa kishairi anaotumia Yeremia kutaja Yerusalemu anapoomboleza kuhusu kuharibiwa kwa mji huo? (Maombolezo 2:2)
8. Daudi alimwogopa mtawala yupi hata akajifanya kuwa na wazimu? (1 Samweli 21:12-15)
9. Kwa nini adhabu ya kifo ilitolewa kwa kutengeneza au kuyatumia mafuta ya kutawaza ambayo Yehova alimwagiza Musa? (Kutoka 30:31-38)
10. Paulo na Barnaba walikuwa na “mfoko mkali wa hasira” kumhusu mwanafunzi yupi, kisha wakatengana na kila mmoja alikwenda njia yake? (Matendo 15:36-41)
11. Kulingana na Yohana 3:16, mtu anaweza kupata uhai udumuo milele kwa msingi gani?
12. Wakristo wa karne ya kwanza waliwaitaje waamini wenzao? (3 Yohana 14)
13. Ni nani aliyetambuliwa kwa namna yake ya kukimbia alipomletea Daudi habari? (2 Samweli 18:27)
14. Kwa nini Musa hakuruhusiwa kuingia katika Nchi ya Ahadi? (Hesabu 20:7-12)
15. Ni nani aliyejulikana kwa kuendesha gari “kwa kasi”? (2 Wafalme 9:20)
Majibu kwa Maswali
1. Kwa sababu Yehova amesema: “Kisasi ni changu; hakika mimi nitalipa”
2. Yeye pekee anastahili kupewa ibada, utukufu na sifa
3. Ulikuwa kama chakula kwake
4. Hebroni
5. Zumaridi
6. Puteoli
7. “Binti Yuda”
8. Akishi, mfalme wa Gathi
9. Yalionwa kuwa matakatifu, hivyo yakiashiria umuhimu na kutengwa tu kwa mambo yaliyoamriwa na Yehova
10. Marko
11. Kudhihirisha imani katika Yesu
12. Marafiki
13. Ahimaasi
14. Alitenda bila kufikiri na hakulisifu jina la Yehova wakati alipowapa Waisraeli maji
15. Yehu