Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Majengo Marefu Yangali Yanajengwa Huko Asia

Majengo Marefu Yangali Yanajengwa Huko Asia

Majengo Marefu Yangali Yanajengwa Huko Asia

Gazeti la The Wall Street Journal linasema hivi: “Kuna mradi wa kujenga majengo sita marefu sana ambayo yatakuwa marefu kuliko jengo la World Trade Center ambalo lilikuwa na kimo cha futi 1,376 [meta 419]. Majengo hayo yote yatajengwa huko Asia.” Gazeti la Journal linaongeza kwamba ‘kwa miaka 20 watu wamependa na wangali wanapenda majengo marefu.’

Majengo hayo marefu sana yatajengwa katika majiji mbalimbali nchini China, Korea, na Taiwan. Cesar Pelli, aliyechora ramani za yale majengo marefu zaidi ulimwenguni kwa sasa, yaani Majengo mawili ya Petronas huko Kuala Lumpur, Malaysia, anasema hivi: ‘Tamaa ya kufika angani imekolea sana katika akili ya wanadamu. Tangu Mnara wa Babeli ulipojengwa, watu wametamani kuweka ishara ya kuwatambulisha angani.’

Wahandisi wanafanya jitihada za kuongeza usalama katika majengo. Hiyo inatia ndani kuacha sehemu wazi baada ya kila orofa 10 hadi 12 ili watu wakimbilie hapo wakati wa dharura, kuimarisha sehemu zenye lifti au ngazi, kuweka vitegemezi ambavyo vinaunganisha sehemu hizo na nguzo kuu za pembeni au zile zinazozunguka jengo. Pia, inahusisha kuongeza ngazi zinazohitajiwa wakati moto unapotokea ghafula ambazo hupanuka kuelekea chini ya jengo ili kutoshea watu wengi zaidi.

Kwa sasa, kuna majengo 24 hivi ulimwenguni pote yenye kimo cha zaidi ya meta 300, ambayo yanatumika, na zaidi ya nusu ya majengo hayo yanapatikana huko Asia. “Hata hivyo, wataalamu wanakubali kwamba hakuna haja ya kuwa na majengo yanayozidi orofa 60,” lasema gazeti la Journal.

[Picha katika ukurasa wa 18]

Majengo ya Petronas ndiyo majengo marefu zaidi ulimwenguni yakiwa na kimo cha meta 452

[Chati/Picha katika ukurasa wa 18]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Urefu wa majengo unatia ndani minara ya kupamba jengo bila kuhusisha nyaya za kupokea mawimbi ya sauti.

Meta 143 Piramidi la Khafre, huko Giza, Misri 2500 K.W.K.

Meta 300 Mnara wa Eiffel, huko Paris, Ufaransa 1889

Meta 348 Jengo la T & C, huko Kaohsiung, Taiwan 1997

Meta 369 Jengo la Benki ya China, huko Hong Kong, China 1989

Meta 381 Jengo la Empire State, huko New York, Marekani 1931

Meta 442 Jengo la Sears, huko Chicago, Marekani 1974

Meta 452 Majengo ya Petronas, huko Kuala Lumpur, Malaysia 1997

Meta 460 Jengo la Shanghai World Financial Center, huko Shanghai,

China (Litajengwa katika 2007)

Meta 508 Jengo la Taipei Financial Center, huko Taipei,

Taiwan (Litakamilishwa kufikia 2003)

[Hisani]

Michoro yote: Courtesy SkyscraperPage.com