Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Baada ya Mfalme Yehoshafati kuanzisha mfumo bora wa hukumu, aliwaamuruje mahakimu kwa kuwa walikuwa wakihukumu kwa niaba ya Yehova wala si mwanadamu? (2 Mambo ya Nyakati 19:7 Biblia Habari Njema)
2. Kwa kuwa Utawala wa Kristo wa Miaka Elfu Moja utakuwa na wafalme wasaidizi walio makuhani huko mbinguni, ni nani watakaomwakilisha hapa duniani na kutekeleza maagizo yake? (Zaburi 45:16)
3. Mitume wote 11 waaminifu wa Yesu walitoka eneo gani? (Luka 4:14)
4. Yoshua aliomba nini kwa niaba ya Wagibeoni waliokuwa wamezingirwa ili Waamori wasipate ushindi? (Yoshua 10:12, 13)
5. Katika Biblia, Bahari ya Mashariki imepewa majina gani tofauti? (Kumbukumbu la Torati 3:17)
6. Kwa nini Hamani alipanga njama ya kuwaua Wayahudi wote katika Milki ya Uajemi? (Esta 3:5, 6, 10)
7. Rabshake, msemaji wa Senakeribu, alitumia ushawishi gani ili kujaribu kumfanya Hezekia asalimu amri? (2 Wafalme 18:33-35)
8. Ni manabii gani wawili waliokuwa mashuhuri wakati wa utawala wa Daudi? (2 Samweli 12:1; 24:11)
9. Mungu aliumba nini katika siku ya pili ya uumbaji? (Mwanzo 1:7)
10. Waisraeli walikuwa wapi Yoshua alipowatuma wapelelezi wawili kwenda Yeriko? (Yoshua 2:1)
11. Ni bidhaa gani zilizotumiwa kutengeneza “mafuta matakatifu ya kutiwa”? (Kutoka 30:23-25)
12. Belshaza aliahidi kumpa zawadi gani mtu ambaye angefasiri mwandiko wa mkono ukutani? (Danieli 5:7)
13. Ni mdudu gani anayejulikana kuwa mwenye bidii na hekima ya kiasili? (Mithali 6:6)
14. Ni mfalme yupi wa Yudea aliyekabili kikosi cha wanajeshi milioni moja ya Waethiopia? (2 Mambo ya Nyakati 14:9, 10)
15. Mpumbavu anayerudia kufanya upumbavu anafananishwa na mnyama gani anayerudia matapiko yake? (Mithali 26:11)
16. Ni mito gani miwili ya Dameski ambayo Naamani aliona ikiwa bora kuliko “maji yote ya Israeli”? (2 Wafalme 5:12)
17. Yesu alishtakiwa kufanya kosa gani kwa sababu alisema angekaa kwa Zakayo, yule mtoza ushuru? (Luka 19:7)
18. Malaika aliwaua Waashuru wangapi katika usiku mmoja? (2 Wafalme 19:35)
19. Petro alisema Mungu aliwapa adhabu gani “malaika waliofanya dhambi”? (2 Petro 2:4)
Majibu ya Maswali
1. “Mwe waangalifu katika kila jambo mtakalolitenda kwa sababu Mwenyezi-Mungu wetu hatavumilia upotoshaji wa haki, wala upendeleo wala rushwa”
2. Wakuu
3. Galilaya
4. Kwamba jua na mwezi zisimame tuli
5. “Bahari ya Araba, Bahari ya Chumvi”
6. Kwa sababu alikuwa Mwagagi, yaelekea Hamani alikuwa uzao wa Waamaleki—ambao walihukumiwa kuangamizwa kabisa kwa sababu waliwachukia Wayahudi
7. Alisema kwamba sawa na miungu ya miji mingine iliyokuwa imetekwa, Yehova hangeweza kuokoa Yerusalemu
8. Nathani na Gadi
9. “Anga”
10. Shitimu, katika nyanda za Moabu
11. Manemane, mdalasini wenye manukato, kane, kida, na mafuta ya zeituni
12. Mavazi ya rangi ya zambarau, mkufu wa dhahabu, na angekuwa mtu wa tatu katika ufalme
13. Chungu
14. Mfalme Asa
15. Mbwa
16. “Abana na Farpari”
17. “Aliingia apate kukaa pamoja na mwanamume aliye mtenda-dhambi”
18. 185,000
19. Walitupwa ndani ya Tartaro