Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kitabu “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Ni vitu gani ambavyo Yehova alisema havitakoma? (Mwanzo 8:22)
2. Ni mimea gani ambayo Yesu alisema kwamba Mafarisayo waliitoa dhabihu, na kukosa kuzingatia “haki na upendo kwa Mungu”? (Luka 11:42)
3. Yesu alisema angerudi kwa njia gani? (Ufunuo 16:15)
4. Samsoni aliwaua Wafilisti wangapi akitumia “mfupa mbichi wa taya ya punda-dume”? (Waamuzi 15:15)
5. Yesu amepewa jina gani kwa kuwa aliumbwa na Yehova moja kwa moja? (Yohana 3:18)
6. Paulo aliwapa Wathesalonike maagizo gani kuhusu watu wavivu? (2 Wathesalonike 3:10, 12)
7. Yesu alisema kwamba watu wote wanapaswa kufanya nini ili ‘waingie kupitia mlango mwembamba’? (Luka 13:24)
8. Ni jiji gani lililohusianishwa na sehemu ya kaskazini zaidi ya Israeli? (1 Samweli 3:20)
9. Mungu alitumia njia gani kuwaonya wale wanajimu waliomtembelea Yesu wasirudi kwa Mfalme Herode? (Mathayo 2:12)
10. Kwa kuwa majina ya cheo hayana wingi yanapokuwa kabla au baada ya jina la Yesu katika Maandiko, ni majina gani ya cheo ambayo hayapatikani?
11. Kwa nini mwangalizi wa kutaniko anahitajika “kuwa na ushuhuda mzuri kutoka kwa watu walio nje”? (1 Timotheo 3:7)
12. Ni wapi ambapo Filipo alimkuta yule towashi Mwethiopia na kumfundisha? (Matendo 8:26)
13. Sauli alipewa adhabu gani kwa kutotii amri ya Yehova ya kuwaharibu Waamaleki wote pamoja na mifugo yao? (1 Samweli 15:23, 26)
14. Kwa nini Abrahamu aliishi sehemu kubwa ya maisha yake akiwa mgeni mwenye kuhamahama? (Waebrania 11:10; 12:22)
15. Baraba aliyeachiliwa na Pilato badala ya Yesu alikuwa amefanya makosa gani? (Luka 23:25; Yohana 18:40)
16. Mwanamume wa Lida aliyekuwa “amelala juu ya kitanda chake kwa miaka minane” kwa sababu alikuwa amepooza ambaye aliponywa na Petro aliitwa nani? (Matendo 9:32-34)
Majibu ya Maswali
1. “Kupanda mbegu na kuvuna, baridi na joto, majira ya kiangazi na majira ya baridi kali, mchana na usiku”
2. Mnanaa na mchicha
3. “Kama mwizi”
4. 1,000
5. “Mwana mzaliwa-pekee wa Mungu”
6. “Ikiwa yeyote hataki kufanya kazi, basi na asile chakula.” “Kwa kufanya kazi kwa utulivu wale chakula ambacho wao wenyewe wanafanyia kazi”
7. ‘Wajitahidi sana’
8. Dani
9. Kupitia ndoto
10. “Bwana Yesu Kristo” au “Mfalme Yesu Kristo”
11. Ili “asianguke katika shutuma na mtego wa Ibilisi”
12. Katika barabara ya jangwani inayotoka Yerusalemu hadi Gaza
13. Yehova alimkataa “asiwe mfalme wa Israeli”
14. Kwa sababu alikuwa anangojea “jiji lenye misingi halisi,” yaani Yerusalemu la mbinguni
15. Uchochezi, uuaji, na wizi
16. Ainea