Je, Wajua?
Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yanapatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa na orodha kamili ya majibu imechapwa katika ukurasa wa 22. Unaweza kupata habari zaidi katika kichapo Insight on the Scriptures, kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.)
1. Farao alisema kwamba Waisraeli walipaswa kuishi katika eneo gani la Misri, na kwa nini eneo hilo lilifaa hasa? (Mwanzo 47:3-6)
2. Ni sifa gani inayoweza kutokeza ugomvi? (Methali 10:12)
3. Yehova anajionyesha akifanya nini ili kuonyesha uzito na kutegemeka kwa ahadi yake kuhusu nchi ya Israeli? (Ezekieli 36:7)
4. Yesu alitumia mfano gani kuonyesha jinsi alivyotamani kuwakusanya wakazi wa Yerusalemu wasiotii? (Mathayo 23:37)
5. Yesu alikuwa mzao wa mwana gani wa Adamu na Hawa? (Luka 3:38)
6. Ni nani waliochochea njama ya kumwua Yesu? (Mathayo 26:3)
7. Kulingana na mtume Yohana, ni mwaliko gani unaotolewa kwa wote ‘wanaoona kiu’ ya uadilifu? (Ufunuo 22:17)
8. Mtu anapaswa kufanya nini ikiwa anahisi kwamba hana hekima, na kwa nini? (Yakobo 1:5)
9. Yehova alifanya nini ili kumtengenezea Adamu mke? (Mwanzo 2:22)
10. Watu watakaokuwa wafalme na makuhani ambao watatawala juu ya dunia pamoja Yesu watatoka katika vikundi gani vya wanadamu? (Ufunuo 5:9)
11. Kwa nini Yehova hakumruhusu Musa kuingia katika Nchi ya Ahadi? (Hesabu 20:10-12)
12. Daudi alifanya nini ili asiuawe na Wafilisti huko Gathi? (1 Samweli 21:12-14)
13. Ili astahili kuwa mwangalizi Mkristo, mtu anapaswa kuepuka mambo gani mabaya? (Tito 1:7)
14. Dario wa Umedi alichangiaje kujengwa upya kwa hekalu la Yehova huko Yerusalemu? (Ezra 6:5-8)
15. Wazazi wanaomwogopa Mungu wanapaswa kuwafundisha watoto wao sheria za Yehova jinsi gani, na lini? (Kumbukumbu la Torati 6:6, 7)
16. Simoni wa Kirene alihusishwaje wakati wa mauaji ya Yesu? (Mathayo 27:32)
17. Yesu alimnukuu Isaya alipokuwa akiwashutumu waandishi na Mafarisayo kuhusu unafiki wa aina gani? (Mathayo 15:8)
18. Taja muujiza wa kwanza wa Yesu na mahali alipoufanya. (Yohana 2:1-11)
Majibu ya Maswali
1. Huko Gosheni, kwa sababu ndilo eneo la Misri lililokuwa na rutuba sana kwa wafugaji wa mifugo. Familia ya Yakobo ilikuwa ya wafugaji wa mifugo
2. Chuki
3. Akiinua mkono wake katika kiapo
4. Kuku anayekusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake
5. Sethi
6. Wakuu wa makuhani na wanaume wazee wa Israeli
7. Waje na ‘kuchukua maji ya uzima bure’
8. “Aendelee kumwomba Mungu, kwa maana yeye huwapa wote kwa ukarimu na bila kushutumu”
9. Baada ya kumletea Adamu usingizi mzito, alichukua ubavu wake mmoja na kuutengeneza kuwa mwanamke
10. Kutoka katika “kila kabila na lugha na watu na taifa”
11. Alikosa kumtakasa Yehova mbele ya wana wa Israeli kuhusiana na muujiza wa maji nyikani
12. Alijifanya mwenda-wazimu, naye mfalme wa Gathi alimwona kuwa mjinga na hawezi kumdhuru yeyote kwa hiyo akamwachilia
13. Awe bila shtaka, asiwe mshupavu, asiwe mwepesi wa ghadhabu, asiwe mlevi mwenye fujo, asiwe mwenye kupiga watu, asiwe mwenye pupa ya pato lisilo la haki
14. Aliamuru ujenzi huo ugharimiwe na hazina ya kifalme, na vyombo vya dhahabu na fedha ambavyo Nebukadneza alikuwa amevipeleka Babiloni virudishwe
15. Wazazi wanapaswa kutumia kila nafasi, iwe katika pindi rasmi au zisizo rasmi, kukazia kikiki kweli ya Neno la Mungu katika mioyo ya watoto wao
16. Alilazimishwa kubeba mti wa mateso wa Yesu
17. Walimheshimu Mungu “kwa midomo yao,” bali moyo wao ulikuwa “umepelekwa mbali” naye
18. Aligeuza maji kuwa divai kwenye karamu ya ndoa huko Kana