Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Watu fulani wamedai kwamba Paulo hakuvunjikiwa na meli kwenye kisiwa cha Malta, kusini ya Sisili, bali kwenye kisiwa kingine. Alivunjikiwa na meli wapi?

Swali hilo linarejelea dokezo la hivi karibuni kwamba mtume Paulo hakuvunjikiwa na meli kwenye kisiwa cha Malta, bali kwenye kisiwa cha Cephalonia (au, Kefallinía) karibu na Corfu katika Bahari ya Ionia, kwenye pwani iliyo magharibi mwa Ugiriki. Maandiko yaliyoongozwa na roho ya Mungu yanatuambia kwamba Paulo alianza safari yake huko Kaisaria akiwa chini ya ulinzi wa ofisa Mroma, Yulio, pamoja na askari wengine na wafungwa wenzake. Kama inavyoonyeshwa kwenye ramani, walisafiri kwa meli hadi Sidoni na Mira. Huko Aleksandria, Misri, walipanda meli nyingine kubwa ya nafaka na kusafiri kuelekea upande wa magharibi hadi Kinido. Hawangeweza kufuata njia inayodokezwa, yaani, kusafiri kupitia Bahari ya Aegea, kupitia sehemu ya kusini kabisa ya Ugiriki, hadi Roma. Pepo kali ziliwalazimisha kusafiri upande wa kusini kuelekea kisiwa cha Krete, chenye fuo ambazo zingeweza kuwakinga. Huko walitia nanga kwenye Bandari Nzuri. Walipoanza ‘kusafiri baharini kutoka Krete,’ meli “ilishikwa na upepo wenye nguvu” na ‘wenye tufani, uitwao Euroakilo.’ Meli hiyo nzito ya nafaka ‘ilirushwa huku na huku baharini’ hadi usiku wa 14. Mwishowe, watu wote 276 walivunjikiwa na meli kwenye kisiwa ambacho maandishi ya Kigiriki ya Biblia Takatifu hukiita Me·liʹte.—Matendo 27:1–28:1.

Katika miaka iliyopita, kumekuwa na madokezo mbalimbali kuhusu utambulisho wa kisiwa cha Me·liʹte. Wengine wamefikiri kisiwa hicho ni Melite Illyrica, ambacho sasa kinaitwa Mljet, na ambacho kiko katika Bahari ya Adriatiki, kwenye pwani ya Kroatia. Lakini haielekei kisiwa hicho ni Mljet, kwa kuwa Mljet kiko upande wa kaskazini na haiwezekani kwamba Paulo alipita huko katika safari yake iliyompeleka hadi Sirakusi, Sisili, kisha pwani ya magharibi ya Italia.—Matendo 28:11-13.

Watafsiri wengi wa Biblia wamefikia uamuzi kwamba jina Me·liʹte linarejelea kisiwa cha Melite Africanus, ambacho sasa kinaitwa Malta. Bandari ya mwisho huko Krete, ambapo meli iliyokuwa imembeba Paulo ilitia nanga iliitwa Bandari Nzuri. Kisha upepo wenye tufani ukailazimisha meli hiyo kwenda upande wa magharibi kuelekea Kauda. Upepo huo uliendelea kuisukuma meli hiyo kwa siku nyingi, na yaonekana kwamba ingesukumwa kuelekea magharibi hadi Malta.

Kwa kufikiria pepo za kawaida katika eneo hilo, na pia “mwelekeo na mwendo wa pepo hizo,” Conybeare na Howson, waliandika hivi katika kitabu chao, The Life and Epistles of St. Paul: “Kisiwa cha Klauda (au, Kauda) kiko umbali wa kilometa zinazopungua 770 kutoka Malta. Jambo hilo ni lenye kutokeza sana hivi kwamba, ni vigumu mtu kuamini kwamba, nchi kavu ambayo mabaharia hao [walikaribia] usiku wa kumi na nne inaweza kuwa si Malta, bali kisiwa kingine. Bila shaka, kisiwa hicho ni Malta.”

Ingawa huenda watu wakataja visiwa vingine, kuvunjika kwa meli kwenye Kisiwa cha Malta kinachoonyeshwa kwenye ramani ndiko kunakopatana na masimulizi ya Biblia.

[Ramani/Picha katika ukurasa wa 31]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Yerusalemu

Kaisaria

Sidoni

Mira

Kinido

KRETE

KAUDA

MALTA

SISILI

Sirakusi

Roma

MLJET

UGIRIKI

CEPHALONIA