Mungu Yuko Wapi?
Mungu Yuko Wapi?
Septemba 11, 2001 (11/9/2001): Mwendo wa saa 2 na dakika 46 asubuhi, ndege ya abiria inagonga jengo la kaskazini la World Trade Center huko New York City, huo ndio mwanzo wa mashambulizi ya kigaidi yaliyopangwa. Kwa dakika 102 zinazofuata, watu 3,000 hivi wanakufa.
Desemba 26, 2004 (26/12/2004)
Tetemeko la nchi lenye kipimo cha 9.0 katika Bahari ya Hindi linasababisha mawimbi makubwa yenye kuua ambayo yanapiga nchi 11, kutia ndani Afrika, umbali wa kilomita 5,000 hivi. Kwa siku moja tu, watu 150,000 wanakufa au kupotea, na zaidi ya milioni moja wanaachwa bila makao.
Agosti 1, 2009 (1/8/2009): Mwanamume mwenye umri wa miaka 42 pamoja na mwanawe wa miaka 5 wanagonga ukuta wa mbao wa bandari wakiwa ndani ya kigari kinachoteleza juu ya barafu. Baba anakufa. Mwanawe anabaki hai lakini anakufa siku inayofuata. Mtu mmoja wa ukoo aliyefadhaika alisema hivi: “Tulitumaini kwamba kungekuwa na muujiza na kijana huyo angepona.”
Unaposoma kuhusu mashambulizi ya kigaidi au misiba ya asili au unapopatwa na msiba, je, unajiuliza ikiwa Mungu anaona yale yanayotukia? Je, unajiuliza ikiwa ametuacha? Biblia inatoa jibu lenye kufariji, kama tutakavyoona.
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]
© Dieter Telemans/Panos Pictures
PRAKASH SINGH/AFP/Getty Images
© Dieter Telemans/Panos Pictures