Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Chagua Marafiki Zako kwa Hekima

Chagua Marafiki Zako kwa Hekima

Njia ya 4

Chagua Marafiki Zako kwa Hekima

BIBLIA INAFUNDISHA NINI? “Anayetembea na watu wenye hekima atakuwa na hekima.”—Methali 13:20.

KWA NINI INAWEZA KUWA VIGUMU? Marafiki zetu wanaweza kutusaidia tuwe na uradhi au tusiwe na uradhi. Mtazamo na maongezi yao yanaweza kuathiri mtazamo wetu kuelekea maisha.—1 Wakorintho 15:33.

Kwa mfano, fikiria simulizi la Biblia kuhusu wanaume 12 waliorudi kutoka kupeleleza nchi ya Kanaani. Wengi wao ‘walizidi kuwaletea wana wa Israeli habari mbaya juu ya nchi waliyokuwa wameipeleleza.’ Hata hivyo, wawili kati yao waliisifu nchi ya Kanaani, wakiiita “nchi nzuri sana, sana.” Lakini mtazamo usiofaa wa wale wapelelezi kumi ulienea kati ya watu. “Kusanyiko lote likapaaza sauti zao,” simulizi hilo linasema, “na wana wote wa Israeli wakaanza kunung’unika.”—Hesabu 13:30–14:9.

Vivyo hivyo leo, watu wengi ni “wanung’unikaji, walalamikaji juu ya fungu lao maishani.” (Yuda 16) Ni vigumu sana kuridhika ikiwa una marafiki ambao hawaridhiki kamwe.

UNAWEZA KUFANYA NINI? Chunguza mazungumzo kati yako na marafiki zako. Je, mara nyingi marafiki hao hujisifu kwa sababu ya vitu walivyo navyo, au nyakati zote wanalalamika kwa sababu ya vitu ambavyo hawana? Nao wanakuona kuwa rafiki wa aina gani? Je, unajaribu kuwafanya marafiki zako wakuonee wivu, au unawatia moyo waridhike na vitu walivyo navyo?

Fikiria mfano uliowekwa na Daudi, ambaye angekuja kuwa mfalme, na Yonathani, mwana wa Mfalme Sauli. Daudi alikuwa akiishi nyikani kama mkimbizi. Mfalme Sauli alihisi kwamba cheo chake akiwa mfalme kilikuwa kinahatarishwa na Daudi na hivyo akataka kumuua. Hata ingawa Yonathani angekuwa mfalme baada ya baba yake, tayari alikuwa mmoja wa marafiki wa karibu wa Daudi. Yonathani alitambua kwamba Mungu alikuwa amemweka rasmi Daudi kuwa mfalme, na aliridhika kumuunga mkono rafiki yake.—1 Samweli 19:1, 2; 20:30-33; 23:14-18.

Unahitaji marafiki kama hao, ambao wanajitahidi kuridhika na wanaokutakia mema. (Methali 17:17) Bila shaka, ili upate marafiki kama hao, wewe pia unahitaji kuwa na sifa nzuri.—Wafilipi 2:3, 4.

[Picha katika ukurasa wa 7]

Je, marafiki zako wanakusaidia uwe na uradhi au usiwe na uradhi?