SEHEMU YA 7
Kufufuliwa kwa Yesu Mpaka Kufungwa kwa Paulo
Siku ya tatu baada ya kufa kwake, Yesu alifufuliwa. Siku hiyo akaonekana kwa wafuasi wake mara tano zilizo tofauti. Yesu akaendelea kuonekana kwao kwa siku 40. Kisha, wengine kati ya wanafunzi wake walipokuwa wakitazama, Yesu akapanda mbinguni. Siku kumi baadaye Mungu alimwaga roho takatifu juu ya wafuasi wa Yesu waliokuwa wakingoja Yerusalemu.
Baadaye, adui za Mungu wakasababisha kufungwa kwa mitume gerezani, lakini malaika aliwafungua. Wapinzani walimpiga mwanafunzi Stefano kwa mawe akafa. Lakini twajifunza jinsi Yesu alivyomchagua mmoja wa wapinzani hao awe mtumishi wake wa pekee, akawa mtume Paulo. Ndipo, miaka mitatu na nusu baada ya kufa kwa Yesu, Mungu akamtuma mtume Petro akamhubiri Kornelio asiye Myahudi na jamaa yake.
Karibu miaka 13 baadaye Paulo alianza safari yake ya kuhubiri. Katika safari yake ya pili Timotheo ajiunga na Paulo. Twajifunza jinsi Paulo na wasafiri wenzake walivyoona mambo mengi ya kufurahisha katika kumtumikia Mungu. Mwishowe, Paulo akafungwa Roma. Miaka miwili baadaye akafunguliwa, lakini akafungwa tena na kuuawa. Matukio ya Sehemu ya 7 yalitukia kwa muda wa miaka kama 32.
KATIKA SEHEMU HII
HADITHI YA 102
Yesu Yuko Hai
Baada ya malaika kuliviringisha jiwe kutoka katika kaburi la Yesu, askari waliokuwa wakilinda walishtushwa na kile walichoona ndani ya kaburi.
HADITHI YA 103
Ndani ya Chumba Kilichofungwa
Kwa nini wanafunzi wake hawakumtambua baada Yesu ya kufufuliwa?
HADITHI YA 104
Yesu Anarudi Mbinguni
Kabla Yesu hajapaa angani, anawapa wanafunzi wake amri moja ya mwisho.
HADITHI YA 105
Kungojea Yerusalemu
Kwa nini Yesu aliwamwagia wanafunzi wake roho takatifu katika siku ya Pentekoste?
HADITHI YA 106
Wanafunguliwa Katika Gereza
Viongozi wa kidini Wayahudi wanawaweka mitume gerezani ili kusimamisha kazi yao ya kuhubiri, lakini Mungu ana mpango mwingine tofauti.
HADITHI YA 108
Wakienda Damasko
Mwangaza unaopofusha na sauti kutoka mbinguni vyabadili maisha ya Sauli.
HADITHI YA 109
Petro Anamtembelea Kornelio
Je Mungu anawaona watu kutoka jamii au taifa moja kuwa bora kuliko wale wa jamii au mataifa mengine?
HADITHI YA 110
Timotheo—Msaidizi Mpya wa Paulo
Timotheo anaondoka nyumbani na kujiunga na Paulo katika safari yenye kusisimua ya kuhubiri.
HADITHI YA 111
Mvulana Aliyelala Usingizi
Eutiko analala usingizi wakati wa hotuba ya kwanza ya Paulo, lakini si wakati wa hotuba ya pili. Kilichotukia katikati ya hotuba hizo ni, muujiza.
HADITHI YA 112
Meli Inaharibika Katika Kisiwa
Mara tu inapoonekana hakuna tumaini, Paulo anapokea ujumbe kutoka kwa Mungu unaompa matumaini.