Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW BROADCASTING

Sakinisha Programu ya JW Broadcasting Kwenye Roku

Sakinisha Programu ya JW Broadcasting Kwenye Roku

Ili kutazama kituo cha JW Broadcasting kupitia Roku, utahitaji kusakinisha programu ya JW Broadcasting kwenye king’amuzi chako cha Roku. Fuata hatua zifuatazo :

 Unganisha King’amuzi Chako cha Roku

King’amuzi chako cha Roku huja na miongozo ya kukusaidia kukitumia na kuunganishwa kwenye intaneti. Baada ya kuunganisha kifaa chako cha Roku, malizia kwa kufuata miongozo iliyoandikwa kwenye skrini.

Taarifa: Utahitaji intaneti kutoka katika kompyuta au kifaa kingine cha mkononi ili kukamilisha hatua hizi.

Utakapoanza, utaombwa uunganishe king’amuzi chako cha Roku. Ili kufanya hivyo, tembelea www.roku.com/link na uingize namba kwenye skrini ya televisheni yako. Halafu fuata mwongozo ulio katika kompyuta yako au kifaa chako cha mkononi kufungua akaunti ya Roku.

Mara tu utakapokuwa umeunganisha king’amuzi chako cha Roku na akaunti yako, utaiona kwenye skrini ya televisheni.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kurekebisha kifaa chako cha Roku, Ona sehemu ya Msaada kwenye tovuti ya Roku.

 Sakinisha Programu ya JW Broadcasting Kupitia Kompyuta

King’amuzi cha Roku kina programu inayoiwezesha kucheza video. Ingiza vipindi vyenye video ambazo ungependa kutazama. Njia moja ya kuweka au kuongeza kipindi kipya ni kwa kutumia kompyuta.

  • Tembelea ukurasa wa JW Broadcasting kwenye kituo cha Roku kwenye intaneti.

  • Fungua akaunti yako ya Roku ikiwa bado haujaifungua.

  • Bonyeza sehemu ya Ongeza Vipindi. Ukikamilisha kufanya hivyo, sehemu ya Ongeza Vipindi iliyo katika rangi ya kijani itabadilika na kuwa Sakinishwa.

Baada ya kuongeza kituo kutoka kwenye intaneti, utahitaji kukisakinisha kwenye king’amuzi chako cha Roku.

  • Bonyeza Mwanzo kwenye kibonyezo chako cha Roku.

  • Tumia kishale kwenda Juu au Chini, kwenda kwenye Mipangilio.

  • Bonyeza OK.

  • Kwenye ukurasa wa Mipangilio, tafuta Mfumo Upya, halafu bonyeza OK. Ukurasa wa Mfumo Upya utafunguka. Utaona sehemu iliyoandikwa Tazama Sasa upande wa kulia wa skrini yako.

  • Bonyeza OK.

King’amuzi chako cha Roku sasa kitatafuta kituo ulichochagua na kukisanikisha.

  • Rudi kwenye ukurasa wa mwanzo wa kin’gamuzi cha Roku na uchague Vipindi Vyangu kutoka kwenye menyu kuu. Ukurasa huu unaorodhesha vipindi vyote ulivyosakinisha katika kifaa chako cha Roku, kutia ndani JW Broadcasting.

  • Nenda kwa alama ya jw.org na bonyeza OK kuanza JW Broadcasting.

 Sakinisha Programu ya JW Broadcasting Kupitia Roku

Unaweza pia kusanikisha JW Broadcasting moja kwa moja kupitia king’amuzi chako cha Roku.

  • Nenda katika sehemu mbalimbali za ukurasa wa mwanzo wa kin’gamuzi cha Roku.

  • Tumia kishale kwenda Juu au Chini kwenye kibonyezo chako cha Roku, na uende kwenye menyu kuu sehemu ya Tafuta.

  • Bonyeza OK.

Sehemu ya Tafuta kwenye Roku inatafuta sinema, vipindi vya televisheni, waigizaji, wasimamizi, michezo, na vipindi vyenye majina yanayofanana na herufi unazoandika. JW Broadcasting ni kituo, hivyo katika orodha hiyo tafuta jina lenye ishara ya Kipindi pembeni. Andika moja wapo ya maneno yafuatayo kuipata JW Broadcasting:

  • jw broadcasting

  • jw.org

  • jwtv

  • Yehova

  • Kituo cha JW Broadcasting kikipatikana kwenye orodha, bonyeza mshale wa Kulia mpaka ulifikie jina la kipindi, halafu bonyeza OK. Sehemu ya Ongeza vipindi itakuwa imemulikwa.

  • Bonyeza OK tena ili kusakinisha JW Broadcasting.

Kutazama JW Broadcasting, chagua Vipindi, au rudi kwenye ukurasa wa mwanzo kwenye kin’gamuzi cha Roku na utafute JW Broadcasting chini ya Vipindi Vyangu.